Please ensure Javascript is enabled for purposes of website accessibility Profile - DR RAPHAEL MWAURA GACHEIYA
Upload

DR RAPHAEL MWAURA GACHEIYA

OffLine
Staff Information
PERSONAL DETAILS
Designation
LECTURER
Corporate Email
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Job Category
Teaching
Phone Number
+254720477709
Division / Faculty
Faculty of Arts and Social Sciences
Directorate / Dept
DEPT. OF LITERATURE, LANGUAGES & LINGUISTICS
Academic-Kiswahili (lugha na Isimu)
Address
14557-20100
SUMMARY

Dkt. Raphael M. Gacheiya alifuzu na Shahada ya kwanza katika Kiswahili na Soshiolojia Kiwango cha daraja la kwanza (1st class Honours) mwaka wa 2003. Alifuzu Shahada ya Uzamili (2007) na Shahada ya Uzamifu (2018) katika Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Egerton. Kwa sasa ni mhadhiri wa Kiswahili na mtahini wa Idara katika Idara ya Fasihi, Lugha na Isimu. Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti na Mshirikishi wa mawasilisho ya shahada za juu Idarani, Mwelekezi, Mshirikishi na Mratibu wa Masomo ya Kiswahili idarani katika ngazi zote za shahada. Amewahi kuwa mwakilishi wa Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii katika Bodi ya Halmashauri ya Shahada za juu, Chuo Kikuu cha Egerton kwa miaka minne. Katika kitengo cha Utafiti na Huduma za Nyanjani, Dkt. Raphael M. Gacheiya ni Msimamizi na mwelekezi wa Mradi wa SCARA unaofadhiliwa na serikali ya Austria (OEAD- Appear).

Dkt. Raphael M. Gacheiya amewahi kuwa mwalimu katika shule za upili na kupanda ngazi hadi kuwa Mkuu wa Idara. Awali alisimamia na kuelekeza miradi miwili  (ROSA na CLARA) iliyofadhiliwa na Muungano wa Ulaya.  Pia ana utalamu wa kutafsiri na ametafsiri kutoka Kiingereza hadi kwa Kiswahili na kuhariri makala ya "Sustainable Sanitation Alliance vision document". www.susana.org. " State of Health and Education among Minority and Indegenous peoples in Kenya", Baseline Study on Indeginous Peoples' Land Rights in Nakuru County"www.ogiekpeoples. Reparations at last: Land justice for Kenya’s Ogiek (www.minorityrights.org)

 

ORCID
https://orcid.org/0000-0002-0939-673X
Researchgate
https://www.researchgate.net/profile/Raphael-Gacheiya
ACADEMIC QUALIFICATIONS

1. 2018: Shahada ya Uzamifu (PhD) katika Kiswahili- Chuo Kikuu cha Egerton

2. 2008: Cheti cha Usafi wa Kiekolojia (Ecological Sanitation)-UNESCO-IHE, The Netherlands

3. 2007: Shahada ya Uzamili (M.A) katika Kiswahili- Chuo Kikuu cha Egerton

4. 2004: Shahada ya kwanza (B.A) katika Kiswahili and Soshiolojia- Chuo Kikuu cha Egerton

5. 1993-1996: Cheti cha Mtihani wa Kitaifa wa Shule za Upili (KCSE)- Utumishi Academy

FIELDS OF SPECIALIZATION

Tafsiri, Mawasiliano na Stadi za Mahusiano mema, Utalamu katika lugha ya Kiswahili na Uhariri, Isimu na nadharia za isimu. (Translation, communication and public relation skills, Competence in Kiswahili language use and Editing, Kiswahili Linguistics and Linguistic Theories)

PROFESSIONAL QUALIFICATIONS

1. 2019: Cheti katika uandishi wa kisanaa, uelekezaji wa maigizo na ukaguzi wa michezo ya kuigiza-KUPAA

2. 2019: Pedagogical Leadership in Africa (PedaL) Training- PASGR

2. 2018: Shahada ya Uzamifu (PhD) katika Kiswahili- Chuo Kikuu cha Egerton

3. 2008: Cheti cha Usafi wa Kiekolojia (Ecological Sanitation)-UNESCO-IHE, The Netherlands

4. 2007: Shahada ya Uzamili (M.A) katika Kiswahili- Chuo Kikuu cha Egerton

5.2004: Shahada ya kwanza (B.A) katika Kiswahili and Soshiolojia- Chuo Kikuu cha Egerton

 

 

WORK EXPERIENCE

Juni 2023 hadi sasa: Msimamizi na Mshirikishi wa programu (Academic Program Leader) ya shahada ya kwanza katika Kiswahili- Chuo Kikuu cha Egerton, Bewa la Njoro.

Juni 2023 hadi sasa: Mwakilishi wa Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii katika Bodi ya Shule ya Masomo ya Juu- Chuo Kikuu cha Egerton, Bewa la Njoro.

Machi 2023 hadi sasa: Mshirikishi, Mratibu na Mwenyekiti wa mawasilisho ya Shahada za juu Idarani. Mshirikishi, mwelekezi na Mratibu wa Kozi na Masomo ya Kiswahili Idarani.

Aprili 2019 hadi 2022: Mwakilishi wa Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii katika Bodi ya Shule ya Masomo ya Juu

Januari 2019: Mwenyekiti Mshikilizi- Idara ya Lugha na Fasihi

Februari 2019 hadi sasa: Mlezi (Patron) wa chama cha Wanafunzi Waigizaji katika kitengo cha Mdiri wa Wanafunzi

2019 hadi sasa: Mhadhiri wa Kiswahili (Isimu ya Kiswahili na Nadharia za Isimu, Tafsiri, Lugha na Mawasiliano, Lugha, Jinsia na Ujinsia)

25.07.2019 hadi 22.08.2019: Mwenyekiti Mshikilizi- Idara ya Lugha na Fasihi

2017 hadi Sasa: Mwanachama katika kamati ya uzingatiaji wa ubora wa huduma na  kamati ya utafiti katika Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii- Chuo Kikuu cha Egerton, Bewa la Njoro.

Juni 2013 hadi 2018: Mhadhiri Msaidizi- Chuo kikuu cha Egerton

2012 hadi sasa: Msimamizi wa maswala ya utahini na mitihani katika Idara ya Fasihi, Lugha na Isimu

2009 hadi 2013: Mhadhiri wa muda Idara ya Fasihi, Lugha na Isimu- Chuo kikuu cha Egerton na Laikipia

Mei 09 – Julai 09: Mtafsiri Mkuu (www.susana.org) Kutafsiri Makala ya Taasisi ya SuSanA (sustainable Sanitation Network) Kutoka Kiingereza hadi kwa lugha ya Kiswahili.

2007 hadi 2013: Msimamizi, mwelekezi na Mshirikishi wa miradi ya ROSA na CLARA katika Chuo Kikuu cha Egerton- Kitengo cha Utafiti. Kuelekeza na kusimamia shughuli za kila siku nchini Kenya na kuwa kiungo kati ya wanamiradi hapa nchini na wafadhili wa Umoja wa Ulaya Uandalizi wa ripoti, uratibu na utekelezaji wa shughuli za uhamasisho na kuwakilisha mradi serikalini na katika vikao vya kitaifa na kimataifa.

2006 hadi 2007: Mwalimu wa Kiswahili na Fasihi na mkuu wa Idara ya Lugha katika shule ya wasichana ya Christ the King Academy- Jimbo Katoliki la Nakuru.

HUDUMA KWA JAMII NA TAASISI ZA JAMII

Juni 2022 hadi sasa: UPPERHILL Secondary School- BOM CHAIRPERSON

Juni 2022 hadi sasa: Nakuru Day Secondary School- BOM Vice Chairperson

Nov 2021 hadi sasa: Kanyiriri Mixed Secondary School; Nyandarua- BOM Member

2019 to date: Gitare Seconday School; Gilgil- BOM Chairperson

Aprili 2012-Mei 2018: St. John The Evangelist Catholic Church; Muguga Nakuru-Church and Parish secretary

Aprili 2013: Catholic Diocese of Nakuru- Translating Novena of the Holy Spirit Book

Dec  2012: Coulson Girls Secondary School- BOM Member

 

KEY PROJECTS

1. Strengthening capacities for agricultural educational research and adoption in Kenya. (SCARA Project). APPEAR OEAD funded project.

2.Capacity-Liked water and sanitation for peri-urban and Rural Areas (CLARA) Project Contract No. 265676), a EU 7th Framework Programme (FP7) funded projects dealing with Water and Sanitation.

 

RESEARCH INTERESTS

Isimu ya Kiswahili na Nadharia za Lugha, Mawasiliano, Tafsiri,Ukalimani na Matumizi ya Lugha, Uchanganuzi wa Diskosi, Usemi na Matini, Matumizi ya lugha katika Midahalo katika tambiko mbadala, nasaha miongoni mwa Wazulufu, Midahalo bishi/tetezi (argumentation) katika miktadha ya kijamii, kidini na kisheria. Peo na Mikakati ya kimazungumzo/malumbano katika mawasiliano anuwai, Lugha, Jinsia na Ujinsia, Lugha na athari zake katika upokezi na uendelevu wa TEHAMA (Teknolojia, Habari na Mawasiliano-ICT).

LIST OF PUBLICATIONS

Gacheiya, R. (2023). A Frame Analysis of President Uhuru Kenyatta’s Madaraka, Mashujaa and Jamhuri Day Speeches. East African Journal of Arts and Social Sciences6(2), 210-225. https://doi.org/10.37284/eajass.6.2.1513

Kitetu, C., & Gacheiya, R. (2023). Protocol and Order during the Mourning Period for the Late President Moi: Understanding Official Discourse of the Disciplined Forces and Cultural Ideologies. East African Journal of Traditions, Culture and Religion6(1), 89-98. https://doi.org/10.37284/eajtcr.6.1.1504

Gacheiya, R. M., Kitetu, C. W. & Chai, J. F. (2022). Discursive Construction of Sexuality among School Going Adolescents in Kenya. East African Journal of Traditions, Culture and Religion, 5(1), 111-121. https://doi.org/10.37284/eajtcr.5.1.967

Gacheiya, R., Chai, J., & Kitetu, C. (2022). “Gari ni Testing”: Uhalalishaji wa Mahusiano ya Kingono Miongoni mwa Wazulufu Nchini Kenya. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili5(1), 388-398. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.878

Ndung’u, P., Gacheiya, R., & Kitetu, C. (2022). Mitazamo ya Lugha na Utambulisho wa Kijamii Miongoni mwa Wazungumzaji wa Kĩndia na Kĩgĩchũgũ. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili5(1), 215-223. (East African Journal of Swahili Studies) https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.769

Mburu, C. K, Abdulrahim, T. na Gacheiya, R. M. (2021). Nadharia ya Metausasa katika Fasihi: Mifano kutoka Shujaaz. Taaluma, Jarida la CHAKITA, 1(1), Uk 35-42. http://chakita.org/makala/nadharia-ya-metausasa-katika-fasihi-mifano-kutoka-shujaaz/

Gacheiya, R, M. Chai, F na Kitetu, C. K. (2020) Mikakati ya Kimazungumzo katika Uumbaji wa Ujinsia wa Miongoni mwa Wazulufu nchini Kenya International Journal of Advanced Research (IJAR)  DOI URL: http://dx.doi.org/10.21474/IJAR01/11428

Gacheiya, R, M na Chai, F. (2020) Ukabila na Uteuzi wa Lugha Vyuoni: Jinamizi la Kitaifa. Journal of Swahili Studies Vol 1:90 https://journals.pu.ac.ke/index.php/jss/issue/view/1 

Gacheiya, R. M. (2020): University cooperation in challenging times: Experiences of SCARA project in Kenya. Oead APPEAR. https://appear.at/en/news/article/2020/10/dealing-with-covid-19-in-university-cooperation

Gacheiya, R. M. (2018): APPEAR in practice_11: The art of mastering e-learning. Oead APPEAR. https://appear.at/en/news/article/2018/12/appear-in-practice-11-the-art-of-mastering-e-learning-1/

Gacheiya, R, M na Chai, F. (2017) “Boy Anayeogopa Sweet Life”: Uwili Katika Uwasilishaji Wa Ujinsia Miongoni Mwa Wazulufu Nchini. RUWAZA AFRIKA Journal of Contemporary Research in Humanities and Social Sciences 5:130-144.

Gacheiya, R. M na Mutua, B.M (2010): Implementation of urine-diversion dry toilets in schools in Nakuru, Kenya. EcoSan Club Schopenhauerstr. 15/8 A-1180 Vienna Austria www.ecosan.at Issue 4: 14-17 

Gacheiya, R.M. and Mutua, B.M., (2009). Sanitation challenges in learning institutions: the case of Nakuru municipality, Kenya. IN: Shaw, R.J. (ed). Water, sanitation and hygiene - Sustainable development and multisectoral approaches: Proceedings of the 34th WEDC International Conference, Addis Ababa, Ethiopia, 18-22 May 2009, 5p.p. https://dspace.lboro.ac.uk/2134/31641http://erepository.kibu.ac.ke/handle/123456789/945

 

CONFERENCES & INVITED PRESENTATIONS

1. Gacheiya, R, M., Kitetu, C na Chai F. (2022). The Death Deodorant: Obituaries in Kenya’s Print Media. Egerton University International Conference.https://conferences.egerton.ac.ke/index.php/euc/article/view/62
2. Gacheiya, R, Kitetu, C na Achieng, B. (2022). A Frame Analysis of President Uhuru Kenyatta’s Madaraka, Mashujaa and Jamhuri Day Speeches of 2020. Egerton University International Conference. https://conferences.egerton.ac.ke/index.php/euc/article/view/56

3. Gacheiya, R, M, Chai, F.  na Kitetu C. (2017) Mikakati ya Kimazungumzo katika Uumbaji wa Ujinsia Miongoni mwa Wazulufu Nchini Kenya-  Kongamano katika Chuo Kikuu cha Rongo.

4. Gacheiya, R, M. na Chai, F. (2017) Karaha ya Ujana: Peo za Kimazungumzo katika Uwasilishaji wa Ujinsia Miongoni mwa Wazulufu Nchini Kenya- The 3rd Eastern Africa Literary and Cultural Studies Conference- University of Dar es Salam.

5. Gacheiya, R, M. na Chai, F. (2017) Discursive Construction of Adulthood: Sexuality and Health in the Church- The 3rd Eastern Africa Literary and Cultural Studies Conference- University of Dar es Salam.

HONORS, PRIZE AND AWARDS

1. HELB Scholarship for M.A

TEACHING AREAS

Isimu-

1. Utangulizi wa Lugha na Isimu

2. Stadi za Mawasiliano na Matumizi Lugha kwa Kiswahili

3. Fonetiki na Fonolojia

4. Msingi wa Sarufi ya Kiswahili

5. Sintaksia ya Kiswahili

6. Tafsiri, Ukalimani, Ufasiri na Unukuzi

7.  Isimu Jamii

8. Semantiki na Pragmatiki

9. Isimu Nafsia.

10. Mofolojia na Mofofonemiki

M.A & PhD Courses

1. Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia

2. Sintaksia, Semantiki na Pragmatiki

3. Tafsiri, Ufasiri, Mawasiliano na Maana

4. Lugha, Uana na Ujinsia 

5. Uchanganuzi wa Diskosi, Usemi na Matini

POSTGRADUATE SUPERVISION
MASTERS LEVEL :

 1. Peris Mwihaki-AM12/14102/15: Lugha na Utambulisho wa Kijamii: Mfano wa Wazungumzaji wa Ki-ndia na Ki-gichugu. (Completed)

2. Achuriatom Kibet- AM12/14103/15: Athari za Kipokot kwa Kiswahili Miongoni mwa Wanafunzi wa Shule za Msingi, Jimbo la Pokot Magharibi.

3. Susan Silantoi- AM12/3795/14: Uchanganuzi wa Makosa Katika Insha za Wanafunzi wa Shule za Msingi Jimbo la Narok Kenya

4. Joyline Jebet Tarus-EM13/09025/20: Analysis of the Relationship between Reading competence and Academic Achievement in Kiswahili  language among Secondary school learners in Baringo central sub-county, Kenya. (Ongoing)

5. Dolvine Kerubo Masagege-AM12/01002/19: Lugha Inayotumiwa Kuzungumzia suala la Mimba za Mapema Shuleni. (Ongoing)

 

PhD. LEVEL :

1. Mburu, Charles Kiarie-AD12/16551/18--Shujaaz: Fasihi ya Stadi za Maisha kwa Vijana Nchini Kenya (Inaendelea)

2. Nancy Chepkemoi Kones-AD12/05003/22: Uongozi Unavyosawirika katika Hotuba za Kampeni za Urais mwaka wa 2022 Nchini Kenya.           (Inaendelea)

 

OTHER SOCIETIES

1. Media Council of Kenya. Member no MCK040180

2.  Kenya Universities Performing Arts and Film Association (KUPAA)-Egerton University Students' Drama and Music Club Patron

REFEREES

1. Prof. Benedict M. Mutua- This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

    Deputy Vice Chancellor,

    Kibabii University

2. Prof. Catherine W. Kitetu- This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

    Associate Professor of Swahili Language and Linguistics

    Department of Literature, Languages & Linguistics,

     Egerton University

3. Rev. Fr. Dr. Gerishon Kuria- This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

    St. Augustine Catholic Chaplaincy,

    Catholic Diocese of Nakuru 

4. Prof. Owen Ngumi- This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

    Founding Dean- School of Education, Arts and Social Sciences

    Zetech University

5Hon Prof. Phylis Bartoo- 0721-768153 This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.  

    Member National Assembly-Moiben Constituency,

    National Assembly, Kenya

Copyright © 2024 Egerton University
"Transforming Lives through Quality Education"