Friday, 20 November 2020 06:25

Nadharia ya Metausasa [Metamordenism] katika Fasihi: Mfano katika Kitabu cha Shujaaz

Written by M. C. Kiarie na A. Taib
Rate this item
(0 votes)

M. C. Kiarie na A. Taib

Idara ya Lugha, Isimuna Fasihi Chuo Kikuu cha Egerton.

Corresponding Author: kiariec90@yahoo.com

 

Fasihi imepitia mabadiliko kadha katika makuzi yake.  Kuanzia fasihi simulizi [hadithi, semi, maigizo, ushairi simulizi, mazungumzo nangomezi], ikaja fasihi andishi [riwaya, tamthilia, hadithi fupi na ushairi andishi] na kasha fasihi ya watoto na vijana inayohusisha michoro.  Kufikia sasa fasihi ipo katika filamu na video. Mabadiliko haya bila shaka yanaandamana na mabadiliko ya namna jamii inavyoendelea kubadilika kijamii, kiuchumi, kiteknolojia na mifumo mingine yajamii. Nadharia za uhakiki wa fasihi nazo zimeasisiwa kukidhi mahitaji haya ya ukuaji haya ya fasihi. Kuna zile nadharia asilia [urasimi, umuundo], nadharia nyambuaji [urasimimpya, umuundoleo] na nadharia changamano [uhalisia, ujamaa]. Nadharia hizi zinatumiwa na zinakidhikika mili fuutunzi na uhakiki wa kazi za fasihi simulizi na fasihi andishi.  Nadharia kama vile ya Usasa [Modernism] baada yake kumetokea nadharia ya Usasa leo [Postmodernism]. Kisha baada ya Usasa leo kuna Metausasa [Metamodernism].  Lengo la utafiti huu ni kuonyesha namna nadharia yametau sasa inavyojidhihirisha katika kazi yafasihi.  Ilikufanikisha haya tutahakiki namna mihimili yake inavyojitokeza katika kitabu cha katuni cha Shujaaz kama fasihi ya kimetausasa. Utafiti huu utafafanua yaliyomo kitabuni hiki kwa kuongozwa na nadharia hii na maelezo na mifano kutolea kitabuni kwa njia ya maelezo. Matokeo yakiwa ni kudhihirisha namna fasihi za kimetau sasa vilivyo kwa kutumia Shujaaz kama mfano.

 

Keywords:

 

Read 101 times

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.